Mark 6:45-50

45 aMara Isa akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 46 bBaada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kuomba.

47 cIlipofika jioni, ile mashua ilikuwa imefika katikati ya bahari, na Isa alikuwa peke yake katika nchi kavu. 48 dAkawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49 elakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, 50 fkwa sababu wote walipomwona waliogopa.

Mara Isa akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!”
Copyright information for SwhKC